Mbunge
 wa Kigamboni Faustine Ndugulile (CCM) amekua akipokea kero mbalimbali 
za wakazi wa Kigamboni ikiwemo kiwango kikubwa cha pesa kinachotozwa 
pale tu wanapopita na magari kwenye daraja hilo, kazifanyia kazi kwa 
kuzifikisha kunakotakiwa na maelezo yake ndio haya hapa chini.
"Kwa
 muda mrefu nimekuwa nikipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na 
huduma isiyoridhisha kwenye Daraja la Nyerere linalounganisha Kigamboni 
na Kurasini.
Malalamiko ya wananchi yako kwenye maeneo makuu matatu:
1.
 Kutumika kwa madirisha machache ya kukatia tiketi. Daraja la Nyerere 
lina madirisha 14 ( Saba wakati wa kuingia na Saba wakati wa kutokea). 
Madirisha yanayotumika ni machache na hivyo kusababisha foleni isiyo na 
msingi.
2.
 Tozo za Daraja la Nyerere zipo juu sana hususan kwa magari ya abiria 
hali hii imepelekea Kigamboni kukosa ruti ndefu za kuelekea maeneo 
mengine ya Jiji la Dar Es Salaam, gari la abiria linatozwa kati ya Tsh 
5000-7000 kwa kila safari ambayo ni gharama kubwa sana kwa kutwa.
3. Kutokamilika kwa kipande kilichobaki toka Darajani hadi kwa Msomali.
Kama
 Mbunge wa Kigamboni nimekuwa nikifuatilia suala hili kwa karibu sana 
bila ya mafanikio, tukumbuke kuwa Daraja la Nyerere lilizinduliwa tarehe
 19.04.2016 na sasa ni zaidi ya miezi 9 hamna kinachoendelea na wahusika
 hawatoi majibu yanayotosheleza.
HATUA NILIZOCHUKUA HADI HIVI SASA
1.
 Mnamo tarehe 15.06.2016 nilimwandikia barua Waziri wa Ujenzi Mhe. 
Makame Mbarawa (Mb) kuhusiana na hoja hizi pamoja na kufatilia zaidi ya 
mara kumi kwa simu, maongezi ya ana kwa ana na meseji, barua yangu 
haijajibiwa hadi hivi sasa (Angalia kiambatanisho).
2.
 Vilevile nilikutana na Mkurugenzi wa NSSF Prog Godius Kahyarara tarehe 
3.10.2016 kuhusu hoja tajwa hapo juu, aliahidi kuchukua hatua za haraka 
lakini hadi hivi sasa hakuna kilichofanyika.
3.
 Kwa kuwa usimamizi wa Daraja la Nyerere upo chini ya NSSF na kipande 
kilichobaki kitajengwa na NSSF, niliomba kukutana na Waziri anayesimamia
 taasisi hii, nilikutana na Waziri Jenista Mhagama (Mb) tarehe 3.12.2016
 ofisini kwake.
"Pamoja na maelezo ya mdomo, nilimkabidhi barua ya malalamiko (Angalia kiambatanisho), Waziri aliahidi kuchukua hatua za haraka.
"Tarehe
 13.12.2016 nilipata nakala ya barua aliyoandika Mhe. Waziri Mhagama 
kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ili kupata maelezo na ufumbuzi wa 
hoja nilizotoa, pamoja na kukumbushia Mhe. Waziri Mhagama hajanipatia 
majibu ya hoja zangu.
"Aidha,
 maelezo niliyopata toka kwa Mkurugenzi wa NSSF wakati Waziri Mkuu 
anatembelea Kigamboni tarehe 04.01.2017 ni kwamba fedha zinazohitajika 
kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kipande kilichobaki ni Tsh 24 Bilioni
 na alinihakikishia kuwa FEDHA HIZO ZIPO.
"Michoro (design) ya barabara hiyo IMESHAKAMILIKA, Mkandarasi kwa ajili ya kazi hiyo YUPO
"Pamoja
 na NSSF kuwa na fedha ya ujenzi wa barabara hiyo, mkandarasi aliye 
tayari na michoro iliyokamilika, kumekuwa na kigugumizi ya lini kazi hii
 itaanza inasikitisha pia kuona Mawaziri hawajibu barua pamoja na 
kukumbushwa mara kwa mara.
"Kinachoendelea
 sasa hakuna lugha nyingine ya kuielezea zaidi ya UZEMBE na 
KUTOWAJIBIKA, naleta taarifa hii kwenu wakazi wa Kigamboni ili nanyi 
mjue kinachoendelea, ninakusudia kuyapeleka malalamiko yenu kwa mamlaka 
ya juu zaidi baada ya mamlaka tajwa hapo juu kushindwa kupata ufumbuzi."




0 comments :
Post a Comment