Dar es Salaam. Idadi ya Watanzania waliofukuzwa Msumbiji imeongezeka
mpaka kufikia 132, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi kutokana
na operesheni ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji haramu.
Akizungumzia suala hilo leo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan
Kolimba amesema operesheni hiyo haijawalenga Watanzania pekee bali raia
wa nchi nyingine walioingia Msumbiji kinyume cha utaratibu.
Dk Kolimba amesema mji wa Montepuez uliopo jimbo la Cabo Delgado una
Watanzania 3,000 wanaoishi huko na kwamba idadi ya watakaoondolewa
inaweza kuongezeka zaidi.
"Tunaendelea kufuatilia tuhuma za baadhi ya Watanzania kwamba
walifanyiwa ukatili wakati wanarudishwa nyumbani ili tujue hatua za
kuchukua. Maofisa wetu wanashirikiana na serikali ya Msumbiji katika
kuhakikisha Watanzania hawapati matatizo katika operesheni hiyo,"
amesema.
0 comments :
Post a Comment