Ligi Kuu ya Wanawake ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hatua ya 6 Bora ambayo
ilikuwa ianze Febrauri 18, 2017 Uwanja wa Karume, imesogezwa mbele kwa
muda wa juma moja.
Ligi hiyo sasa itaanza rasmi
Februari 26, 2017 kwenye uwanja huohuo wa kumbukumbu ya Karume, Ilala
mahali zilipo ofisi za TFF. Hii ni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya
uwezo wetu.
Timu sita zilizofanikiwa kufika
hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya
Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B”
zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo,
kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa
kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es
Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine
utaanza saa 10.00 jioni.
Ratiba mpya inaonesha kwamba siku
ya Februari 26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na
Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya
Fair Play na Sisterz.
Ratiba kamili kwa mechi
inazofuata itatolewa wiki ijayo. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza au unaoweza
kujitokeza kutokana na mabadiliko hayo
0 comments :
Post a Comment