Kamanda wa polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao hawapokei simu wakidhani wakipigiwa itakuwa ni suala la dawa za kulevya.
Kamanda Sirro ameyasema hayo Jumatano hii katika mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambapo leo ametimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe na Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Amesema, “Awali ya yote Kwanza nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kutimiza mwaka mmoja lakini pia nimpongeze kwa kuwaleta vijana wetu hasa wale waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya.
Kwangu ni siku ya furaha kwasababu tangu hili zoezi lianze hata nikiwapigia simu wasanii kama wakina Banana Zoro hawapokei simu, hata viongozi wa dini hivyo hivyo lakini hii inaonesha kwamba kila mtu anajua umuhimu wa suala hili.”
0 comments :
Post a Comment