Mavugo Afunguka Mazito Mpango Wa Simba Kuchukua Ubingwa



Straika nyota wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, ni kama amepania baada ya kutoa kauli ya kishujaa akitamka kuwa watashinda mechi zote sita walizozibakiza kwenye Ligi Kuu Bara.


Kwa maneno hayo, maana yake Yanga ambao ndiyo wapinzani wao wakubwa wasahau kabisa kuhusiana na suala la kutetea ubingwa wao.


Simba hivi sasa inaoongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 55, Yanga wakifuatia na pointi 53 huku Azam wakiwa wa tatu wenye 44.


Mechi sita ambazo imezibakiza Simba ni dhidi ya Mbao FC, Toto Africans, Kagera Sugar, Mwadui FC, Stand United na African Lyon.

Mavugo alisema hakuna mechi nyepesi kwao kati ya hizo walizozibakiza, lakini kwa pamoja watapambana kuhakikisha wanashinda zote.

Mavugo alisema watalazimika kushinda mechi hizo zote kwa lengo la kutowaruhusu Yanga wawapite au wawakaribie kwenye idadi ya pointi walizonazo kwa hofu ya kuongeza ugumu.

Aliongeza kuwa, ana matumaini ya kushinda mechi hizo kutokana na ubora wa kikosi chao na morali iliyokuwepo kwenye timu kuhakikisha ubingwa wanauchukua kwenye msimu huu.

"Kila timu inakuwa ina mikakati yake, lakini kwetu Simba tulichopanga hivi sasa ni kushinda mechi zote sita tulizobakiza katika msimu huu wa ligi kuu.


"Ninajua siyo kazi rahisi, lakini bidii na kujituma kwetu ndiyo kutafanikisha hayo yote, ninaamini tuna kikosi bora kitakachofanikisha hayo yote.

"Kingine ni umoja na mshikamano uliopo hivi sasa katika timu yetu kwa kuanzia kwa viongozi, benchi la ufundi na wachezaji hatuwezi kuacha pointi hata moja kwa kuwa wapinzani wetu wanakuja kwa kasi," alisema Mavugo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment