Yanga Kuifuata Zanaco FC,Huku Ikiwakosa Washambuliaji Wake Wote

YA
SUALA la majeruhi limekuwa ni tatizo kubwa sana katika kikosi cha Yanga hivi karibuni huku safu ya ushambuliaji ikiathiriwa zaidi kwa nyota wake kadhaa kulazimika kukosa michezo muhimu wakiugulia maumivu.
Usiku wa kuamkia leo uongozi wa timu hiyo umetoa orodha ya wachezaji watakaosafiri kuelekea Zambia katika mechi ya marudiano dhidi ya Zanaco FC huku ikiwakosa washambuliaji wake wote ambao Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Mateo Antony, Malimi Busungu.

Donald Ngoma (kushoto) anaachwa jijini Dar kwa ajili ya kuendelea na matibabu

Kutokana na hali hiyo Yanga italazimika kuwatumia Obrey Chirwa na Emmanuel Martin kama washambuliaji wa latika ingawa kiasili nyota hao wawili ni mawinga na mara nyingi wamekuwa wakifanya vizuri zaidi pale wanaposhambulia kutokea pembeni.
Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka leo jioni majira ya saa 11:15 kwa ndege ya shirika la Kenya Airways.

Kikosi cha Yanga kilichoanza katika mchezo wa awali uliopigwa jijini Dar, Ngoma pekee ndiye atakosekana.

Kikosi kamili kinachoondoka ni kama ifuatavyo;
MAKIPA;
Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ali Mustafa ‘Barthez’.
WALINZI ;
Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.
VIUNGO;
Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Justine Zulu, Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimon Msuva na Geofrey Mwashiuya.

Chirwa na Msuva wanabakia kuwa roho ya Yanga katika kuhakikisha Zanaco inaondolewa mashindanoni

WASHAMBULIAJI;
Obrey Chirwa na Emanuel Martin.
Wachezaji watakaoukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali zikiwemo majeruhi ni Malimi Busungu, Mateo Antony , Pato Ngonyani , Amisi Tambwe , Yusufu Mhilu na Donald Ngoma.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment