Tanzanite:Amponda Diamond......!



Kukumbusha tu Tanzanite alipata jina miaka kadhaa iliyopita baada ya kuurudia wimbo wa Diamond, Mbagala na kudai ulikuwa wake huku pia baadaye akimtuhumu kumroga. Shutuma hizo zilimkera sana Diamond. “Nakutanaga naye [Diamond] lakini si mtu ambaye labda ananipa ushirikiano,” Tanzanite ameiambia Bongo5.

Muimbaji huyo amedai kuwa ugomvi wake na Diamond hadi leo unamwathiri kiasi cha baadhi ya wasanii kukataa kufanya naye kazi.

 “Lakini pia kitu ambacho kinanishangaza kwamba dah sijui labda tasnia yetu inaenda wapi, sijui sisi Watanzania tunakuwa na roho gani. Kwasababu ile kitu niliyofanya, inafika time sasa hivi kuna msanii nataka nifanye naye kazi anakataa kwasababu hiyo,” ameeleza. 

“Yupo msanii ambaye niliwahi kutaka kushirikiana naye akasema ‘bwana mimi naogopa uligombana na jamaa [Diamond]. Mimi sijafanya kitu kibaya kiukweli. Ukiangalia cover ni vitu ambavyo vinafanyika, sijui kibaya kilikuwa ni nini.” Tanzanite aongea kwa uchungu na kudai Diamond aache roho ya kinyongo Kwani ni roho Mbaya.. Anahitaji wamalize tofauti. 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment