AfDB kutoa mkopo ujenzi wa reli ya kati Tanzania

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kushirikiana na Tanzania kujenga mradi mkubwa wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (SGR) kwa kuipatia mkopo wenye masharti nafuu.
Ahadi hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo anayesimamia kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.
Dkt. Weggoro amesema kuwa benki yake imeridhika na utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na rais Magufuli na hivyo kuifanya bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo kukubali kufanikisha ujenzi wa reli hiyo kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
“Benki iko tayari na inasubiri Tanzania ilete mapendekezo ama maombi ili yafanyiwekazi, tutakaa pamoja ili tuone benki itasaidia kiasi gani na benki pia inaweza kuwatafuta wadau wengine tunaosaidiana nao katika miradi mikubwa kama hii,” aliongeza Dkt. Weggoro
Mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge), yenye urefu wa kilometa 2,561 umepangwa kugharimu kiasi cha dola bilioni 7.6 za Marekani, sawa na shilingi za Kitanzania trilioni 16, awamu ya kwanza imeanza kujengwa kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro na baadaye awamu nyingine zitafuata.
Aidha, Dkt. Weggoro amesema benki yake itashirikiana na serikali kuboresha utendaji kazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hususan kwa upande wa muundo wake na madeni makubwa yanayolikabili shirika hilo ili liweze kuchangia ipasavyo ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake Dkt. Kijaji amesema kuwa uwekezaji wa AfDB nchini umefikia Dola bilioni 1.8 huku asilimia 74.5 za uwekezaji huo ukienda kwenye sekta ya miundombinu, ambapo barabara imechukua asilimia 51.4, Nishati (10.1%), Maji na Usafi wa Mazingira (13%) na Sekta nyingine za huduma za jamii, kilimo na masuala ya fedha (25.5%).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment