Baada ya kuichapa Stand United ‘Chama la Wana’ na kushika usukani katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC ‘Wekundu wa Msimbazi’ Jumatano hii Septemba 4, watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Dodoma FC katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mechi hiyo ambayo itaikutanisha Simba na kocha wake wa zamani Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ambaye ndiye kocha wa Polisi FC, ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa raundi ya sita dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Oktoba 14, mwaka huu.
Mchezo huo pia ni sehemu muhimu ya kocha wa Simba, Joseph Omog kutathimini kikosi chake katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA, huku Dodoma FC ya Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ yenyewe ikijipanga zaidi na ligi daraja la kwanza Tanzania Bara



0 comments :
Post a Comment