Bujumbura, Burundi
Kumetokea
ufyatulianaji wa risasi na milipuko usiku kucha nchini Burundi, usiku
wa kuamkia uchaguzi wa rais uliozua utata. Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo
anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na
katiba ya nchi.
Viongozi wengi wa upande wa upinzani wameapa kususia uchaguzi huo.
Saa
chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya
gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi.
Maeneo mengine risasi hizo zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo. Japo
haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo.
Kwa mujibu wa mshauri wa kisasa wa rais, haya ni mashambulio yanayofanywa na 'magaidi' wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi.
Kumbu kumbu
Mnamo
mwezi Mei, kundi la wanajeshi wa ngazi ya juu nchini Burundi walijaribu
kufanya mapinduzi yaliyotibuka. Hata hivyo sasa baadhi yao wametishia
kufanya shambulio lingine.
Hofu ya
kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya
zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa
uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani.
Wito kama
huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani
yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa
kwake ukipuuziliwa mbali.
Takriban
watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huuhuku
wengine zaidi ya elfu 160 wakiikimbia nchi kwa hofu ya kuzuka mapigano.


0 comments :
Post a Comment