Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea, Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea na matibabu.
Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea, Steve Massaburi akiwa
Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea kuuguza majeraha baada ya
kujeruhiwa kwa mapanga nyumbani kwake Segerea jijini Dar es Salaam jana
na watu wasiojulikana. Kushoto anayemuhudumia ni jamaa yake Martin
Pemba.
Na Dotto Mwaibale
WATU wasiojulikana wamejeruhi kwa mapanga Katibu wa Uchumi na Fedha Kata
ya Segerea Steve Massaburi usiku wa kuamkia juzi nje ya nyumba yake
alipokua akirejea kutoka matembezini.
Kwa mujibu wa Steve aliyelazwa katika Hospitali ya Aga khan, watu hao
wapatao wanne wakiwa na Pikipiki, walimvamia majira ya saa tatu usiku
nje ya geti la nyumba anayoishi na kuanza kumshambulia huku yeye
akijaribu kupambana nao.
Steve ambaye ni mtoto wa Meya wa Jiji la Dar es salaam Dk. Didas
Massaburi, alisema wakati watu hao wakimshambulia walikuwa wakisema wazi
wazi kuwa lengo lao ni kumuona hagombei nafasi ya udiwani katika Kata
hiyo ya Segerea baada ya yeye kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi
hiyo.
“Walikuwa wakiniambia kuwa wewe si unautaka udiwani sasa utaugombea
ukiwa kitandani au kaburini, hapa hakuna na umaharufu wa mtu kwa kuwa
kila mtu anaitaka nafasi hiyo” alisema Massaburi.
Alisema wakati akiendelea kupambana na watu hao alikuwa akipiga kelele
jambo lililowafanya watu hao kumuacha na kasha kukimbia huku yeye akiwa
amelala chini damu zikimtoka sehemu za shavuni kutokana na panga
alilopigwa.
Pamoja na sehemu ya shavuni, watu hao pia wamemjeruhi sehemu mbalimbali
za mkono wake wa kushoto alipokuwa akijaribu kuzuia panga kumdhuru
sehemu za usoni.
“Kelele nilizopiga ndizo zilizonisaidia kwa kuwa ziliwafanya watu watoke
katika majumba yao kuja kunisaidia wakati huo huo watu hao wakikimbia
kwa kutumia pikipiki zao mbili walizokuwa wamekuja nao” aliongeza.
Alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri tangu alipofikishwa
hospitalini hapo jana huku akishonwa nyuzi zaidi ya ishirini katika taya
lilipigwa na panga na watu hao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
0 comments :
Post a Comment