Mhifadhi
Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akimpokea
muigizaji maarufu wa filamu wa nchini Afrka Kusini,Jacky Devnarain
maarufu kama Rajesh Kumar ,jina alilotumia katika tamthiliya ya Isidingo
the Need aliposhuka yeye na wenzie 37 waliopanda mlima huo kwa lengo la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wasichana wanaotoka katika
familia maskini.
Mhifadhi
Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya
akimpatia kinywaji ,Muigizaji Jacky mara baada ya kufika katika lango la
Marangu ,akishuka kutoka Mlima Kilimanjaro.

Muigizaji
Jacky akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za
Taifa,Tanzania (TANAPA)Ibrahim Musa baada ya kushuka kutoka Kilele cha
Uhuru ambako kati ya watu 37 waliopanda mlima huo ,32 ndio waliofanikiwa
kufika kileleni.
Mkuu
wa wiaya ya Siha ,Dkt Charles Mlingwa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla
fupi ya mapokezi ya ugeni huo ulioanda mlima Kilimanjaro akimkaribisha
keki Muigizaji Jacky mara baada ya kuteremka kutoka Mlima Kilimanjaro.

Washiriki
wa timu hiyo iliyopanda mlima Kilimanjaro kwa uratibu wa Mfuko wa
Mandela wakifika katika lango la Marangu mara baada ya kushuka kutoka
mlima Kilimanjaro.
Miongoni mwa wapandaji hao alikuwemo Ofisa Uhusiano wa nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom,Maya Makanjee.
Makanjee akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wenzake wa zoezi hilo mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro.

Washiriki
wa zoezi hilo wakifurahia Keki iliyopambwa kwa rangi za Bendera ya
taifa la Afrika Kusini,na Baba wa taifa hilo,Mzee Nelson Mandela
akisalimia.

Mhifadhi
Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ,Erastus Runguro akizungumza
jambo na muigizaji ,Jacky Devnarain (Rajesh Kumar).

Muigizaji Jacky akisindikizwa na Mhifadhi ,Charles Ngendo kupata sehemu ya kupumzika kwa muda .


Muigizaji Jacky (Rajesh Kumar ) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Tanzania,Ibrahim Musa ,
Keki
maalumu iliyotengenezwa na kupambwa kwa rangi za Bendera ya Taifa la
Afrika Kusini iliyokabidhiwa kwa washiriki wa zoezi la kupanda Mlima
Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya familia maskini.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.












0 comments :
Post a Comment