Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akisalimiana na
Diwania wa Kata ya Bwilingu Bw, Ahmed Masser wakati alipowasili katika
eneo la mkutano uliofanyika mji mdogo wa Chalinze jana ukiwa na lengo la
kuelezea utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM uliofanywa na Mbunge
huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja katika huduma za Afya, Elimu, Maji,
Miundombinu, Uchumi, Michezo na amaendeleo mengine ya kijamii.
Mh. Ridhiwania Kikwete ametanganza rasmi jana katika mkutano huo nia
yake ya kutetea jimbo la Chalinze ambapo leo mchana anatarajiwa kuchukua
fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Bagamoyo tayari kwa kuanza mchakato
wa kuwania tena ubunge wa jimbo la Chalinze ili kuendeleza yale
aliyokwishayaanza kutekeleza katika kipidi cha mwaka mmoja alipokuwa
madarakani.
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akisalimiana na
wananchi mbalimbali wakati alipowasili katika eneo la mkutano mjini
Chalinze.
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo
na Katibu wake Bw. Idd Swala huku Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed
Nasser akisikiliza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bw.ndugu Majid
Mwanga.
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga.
Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza na
wananchi mjini Chalinze wakati alipotangaza nia yake ya kutetea tena
ubunge wa jimbo hilo.
Wananchi wa Chalinze wakimsikiliza Ridhiwania Kikwete mbunge wa
jimbo hilo hayupo pichani wakati alipokuwa akitangaza nia yake ya
kutetea tena kiti cha ubunge wa jimbo la Chalinze.


0 comments :
Post a Comment