Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (wa pili kutoka kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Lukas Pub jijini Dar.
Ilikuwa
noma sana siku ya Ijumaa iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi
mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo uje kuona vitu vitamu kutoka
kwenye Bendi ya Skylight
Mashabiki wa Bend ya Skylight wakiendelea kuserebuka.
Sony Masamba akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake ndani ya kiota kipya cha Lukas kilichoko Masaki jijini Dar.
Sakata rhumba na Skylight band hapana chezea hatareee ukigusa lazima unase
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight Shuu akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ( hawapo pichani) uku akisindikizwa na waimbaji wenzake Sony Masamba (kushoto) pamoja na Ashura Kitenge.(kulia)
Katika bend ya Skylight ni full burudani.
Skylight
Band ni mwendo wa kutoa raha sana tukutane Ijumaa hii ndani ya kiota
cha Lukas pub Masaki jijini Dar kwa kuburudika na band hii
Ndani ya Skyligt band ni full burudani.
Ilifika
time ya Nigeria Flavour….. Sam Mapenzi akitoa burudani huku
akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu
kwenye ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto),
Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Mashabiki wakiendelea kuserebuka nyimbo za Skylight.
0 comments :
Post a Comment