Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly mwenye fulana
nyekundu wakifanya maongezi na Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaifa Bi. Rosemery Jairo siku Viongozi
wa Jumuiya ya Watanzania DMV na washirika wao wakiwemo manesi na
madaktari wa kujitolea walipowasili Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma
za kitabibu na madawa bure katika hospitali mbalimbali Tanzania.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Idd Sandaly akiwa katika picha ya
pamoja na mama Mukami walipokutana katika hospitali ya Mwananyamala leo
Jumamtatu July 20, 2015 Uongozi wa DMV na washirika wake walipokwenda
kutoa huduma za kitibabu na msaada wa madawa ya bure.

Kushoto ni Joha Nyang'anyi akisaidia kupaki madawa siku ya Alhamisi
July 16, 2015 Greenbelt, Maryland kabla ya kusafirishwa kuelekea
Tanzania na Jumuiya ya Watanzania DMV wakiwemo washirika wake
wakujitolea. Kulia ni Dr. Sylivia Dassi ambaye ni mmoja wa madaktari
waliojitolea kwenda Tanzania kutoa huduma za kitabibu katka hospitali
mbalimbali Tanzania.

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV na washirika wake wakiwa kwenye
basi kuelekea hospitali ya Mwanannyamala mapema leo Jumatatu July 20,
2015.

Kundi la vijana la DMV lililojitolea kushiriki katika zoezi hili
likipata picha ya pamoja wakiwa hospitali ya Mwananyamala mapema leo
Jumatatu July 20, 2015. Kati ni Asha Nyang'anyi ambaye nae yupo kwenye
msafara huo.








0 comments :
Post a Comment