Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akiwakaribisha nchini
Timu ya Madaktari kutoka Marekani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni.
Madaktari hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa
magonjwa mbalimbali katika Hospitali za Mwananyamala ya Jijini Dar es
Salaam na Mnazi Mmoja, Zanzibar. Ziara ya Madaktari hao ambao wametoka
Washington DC, Maryland na Virginia imeratibiwa na Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Jumuiya ya
Watanzania DMV.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bw. Iddi Sandaly (watatu toka
kulia)ambaye amefuatana na Madaktari hao kutoka Marekani akielezea jambo
mara baada ya kuwasili nchini.
Bibi Jairo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu dhumuni la ziara ya madaktari hao hapa nchini.
Mmoja wa Madaktari kutoka Marekani akizungumza na Waandishi kuhusu ziara yao hapa nchini
Bw. Idd Sandaly akifafanua jambo kwa waandishi kuhusu ziara ya madaktari hao kutoka Marekani.


0 comments :
Post a Comment