nkupamah media
Wakati
Chama cha Mapinduzi kinapinga uamuzi wa Marekani wa kusitisha msaada
kwa Tanzania wa tilioni 1.5 kutokana na kufutwa kwa matokeo ya Uchauzio
Mkuu wa Zanzibar, Chama cha Wananchi CUF kimeunga mkono uamuzi huo na
kutaka mshindi wa urais wa Zanzibar atangazwe na kuapishwa ili kuondoa
vikwazo vya kiuchumi.
Msimamo
huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wananchi
(CUF), Ismail Jussa Ladhu jana alipokuwa akizungumzia uamuzi wa
Marekani kuzuia fedha za MCC hadi muafaka wa uchaguzi utakapopatiwa
hufumbuzi pamoja na kuondoa sheria kandamizi ya makossa ya mitandao.
Jussa
alisema hakuna njia ya kunusuru Tanzania kuwekewa vikwazo vya kiuchumi
ikiwemo kunyimwa misaada zaidi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar kukubali
kukamilisha uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu.
Aidha
alisema kuwa uamuzi wa Marekani wa kuzuia msaada unatoa fundisho kubwa
kwa nchi nyigine kuheshimu mashariti ya kunufaika na fedha za MCC
ikiwemo kulinda misingi ya Demokrasia na Utawala bora.
Jussa
alisema matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar yalifutwa kwa ubabe na
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar baada ya kuona CCM wapo katika
hatari ya kuanguka lakini hakuna kifungu cha Katiba kinachompa uwezo
huo.
Alisema
msimamo wa CUF utaendelea kubakia palepale pamoja na kufanyika kwa
mazungumzo ya kutafuta muafaka wa uchaguzi, ZEC warudi kazini
wakamilishe kuhakiki na kutangaza matokeo na mshindi wa uchaguzi wa
Oktoba 25 mwaka huu.
Alisema
kuwa kuna kikundi cha watu wachache Zanzibar ndiyo hawataki kuona
mabadiliko yakitokea ya kiutawala Zanzibar licha ya CCM kushindwa
kufikia malengo ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
“Kuna
kikundi cha watu Zanzibar hakitaki kuona mabadiliko ya kiutawala kwa
maslahi yao binafsi licha ya CCM kuanguka katika uchaguzi wa Oktoba 25
Mwaka huu,”alisema Jussa.
Alisema
kuwa kadhia ya uchaguzi wa Zanzibar imesababisha madhara makubwa
ikiwemo wananchi kuishi katika mazingira ya wasiwasi pamoja na kupanda
kwa gharama za maisha visiwani humo.
Jussa
alisema hakuna sababu kwa Viongozi wa CCM kuwa na wasiwasi wa kupoteza
vyeo wakati marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar yameweka mfumo
mzuri wa kuunda serikali ya pamoja na wao kunufaika kama CUF
ilivyonufaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Aidha,
alisema CUF haiko tayari kuona Uchaguzi Mkuu unarudiwa Zanzibar kwa
malengo ya kuibeba CCM licha ya kuanguka katika uchaguzi wa awali
Visiwani humo.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, alisema kuwa haikuwa mwafaka
kwa Marekani kuzuia msaada huo wakati Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
ilikuwa na hoja za msingi za kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba
25 Mwaka huu.
Alisema
kuwa uchagfuzi wa Oktoba 25 Mwaka huu ulipoteza sifa za kuwa uchaguzi
huru na wa haki baada ya kutawaliwa na vitendo vya udaganyifu kinyume na
misingi ya demokrasia na utawala bora.
Alisema
hana wasiwasi na Marekani kuwa hawajapata taarifa na vielelezo vya
kuharibika kwa uchaguzi wa Zanzibar na iwapo watapata taarifa hizo
watakubaliana na uamuzi wa ZEC wa kufuta matokeo ya uchaguzi huo.
Alisema
uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya udaganyifu ikiwemo idadi ya
wapiga kura kuzidi watu waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura wa
kudumu pamoja na mawalaka wa vyama kupigwa na kufukuzwa katika vituo vya
kazi.
“Ufumbuzi
wa migogoro sio kuzuia misaada kwa sababu unawaumiza hadi watu
wasiokuwa na hatia, cha muhimu ni kutafuta njia ya mufaka za kuondoa
matatizo.”alisema Vuai.
0 comments :
Post a Comment