nkupamah media
Harakati
za kuwasaka wabadhirifu wa fedha za umma ili waingie kwenye msululu wa
opareshini ya kutumbua majipu iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano
zimeibua tuhuma nyingine zinzomhusu moja kati ya vigogo anayeiwa kuwa
mfanyakazi wa Ikulu.
Taarifa
zilizochapishwa katika gazeti la MwanaHalisi zinaeleza kuwa uchunguzi
uliofanywa na gazeti hilo umebaini nyaraka zinazoonesha kigogo huyo
alitumia fedha za walipa kodi kiasi cha shilingi 821,997.24 kwa ajili ya
kufanyiwa huduma ya kukandwa mwili (massage), katika hotel ya kifahari
ya Four Seasons Safari Lodge iliyoko ndani ya mbuga za wanyama za
serengeti, Arusha.
Kwa
mujibu wa gazeti hilo, stakabadhi waliyoipata katika hotel hiyo
ilionesha kuwa kigogo huyo alifika hotelini hapo April 17 mwaka huu
tarehe ambazo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa na ziara jijini
Arusha.
Imeelezwa
kuwa kigogo huyo ambaye hotel hiyo haikutaka kumtaja jina alilala
katika chumba namba 9017 na alikuwa na mrembo wake ambaye kwa pamoja
walipata huduma zilizoingizwa kwenye stakabadhi iliyolipiwa na Ikulu.
Mbali
na huduma ya Massage, huduma nyingine zilizoorodheshwa nakala ya ankara
hiyo ni usafi wa nguo ambao uligharimu shilingi 676,000.
Katika
kutafuta kujiridhisha, gazeti hilo lilimpigia simu afisa wa hotel ya
Four Seasons Safari Lodge ambaye licha ya kukataa kutoa maelezo alikiri
kuwapokea baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu katika siku tajwa.
Chanzo: Mwanahalisi
0 comments :
Post a Comment