RUANGWA,Lindi
SERIKALI imekwishatenga kiasi
cha sh. bilioni 137 kwa ajili ya kugharamia utoaji wa elimu ya bure
kuanzia Januari hadi Juni, mwakani.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa wakati
akizungumza na mamia ya wananchi waliofika
kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
uwanja wa mikutano wa Likangala wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.
“Kazi ya utumbuaji
majipu imezaa matunda kwani tumeweza kupata fedha za kugahrimia elimu
ya bure ambayo iliahidiwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wakati
wa kampeni. Fedha hiyo tunayo, na tumeshaanza kuisambaza kwa sababu
tunataka shule zikifunguliwa Januari, 2016 watoto waanze kufaidika,” alisema huku akishangiliwa.
“Atakayezigusa
fedha hizi na kuzitumia vibaya ni lazima tutamtumbua tu! Tumeshawapa
maelekezo Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Elimu wao na
kuwaonya kuhusu matumizi ya fedha hizo,” alisema.
“Hatuhitaji
mwanafunzi achangishwe hela ya mitihani, na zile shilingi 10,000/- kwa
ajili ya wanafunzi wanaosoma Sekondari nazo pia tutazipeleka. Na huu ni
mpango wa dharura ambao haukuwemo katika bajeti ya mwaka 2015/2016, kwa
hiyo tutalazimika kuziombea kibali,” alisema.
0 comments :
Post a Comment