MUNICH,Ujerumani
KOCHA wa mabingwa wa Ujerumani,Bayern
Munich,Pep Guardiola amesema kuwa ataamua mustakabali wa maisha yake
ndani ya klabu yake ndani ya msimu ujao.
Kocha huyo ambaye kwa sasa ndiye bidhaa
adimu katika soka la Ulaya kwa upande wa makocha
,amesema kuwa bado
hajafikiria ni nini kitafuata baina yake na klbau hiyo ambayo amejiunga
nayo katika misimu minne iliyopita.
Amesema kuwa anaamini maamuzi
atakayochukua juu ya hatma yake katika klabui hiyo yatamfurahisha kila
mmoja huku akisisitiza kuwa hatafurahishwa kama kuna upande utahuzunika
kwa mamamuzi hayo.
Taarifa za ‘chini ya kapeti’ zinasema
kuwa huenda kocha huyo akaamua kutoongeza mkataba wa kuendelea kuifunza
timu hiyo ambayo imekuwa bingwa katika kipindi chote ambacho amekuwa
nayo nchini Ujerumani.
Aidha taarifa zinasema kuwa huenda kocha
huyo wa kukumbukwa katika klabu ya Fc Barcelona akajiunga na moja wapo
ya timu kubwa za Uingereza huku timu toka jiji la Manchester zikipewa
nafasi kubwa ya kumsaini.
Taarifa nyingine zinadai kuwa Klabu hiyo
imeanza mazungumzo ya chini chini na aliyekuwa kocha wa Madrid,Carlos
Ancelotti kwa ajili ya kwenda kuinoa timu hiyo endapo Pep atatangaza
kuhama katika timu hiyo.
0 comments :
Post a Comment