DAR ES SALAAM
Jumla ya Wanafumzi 7I0 wa shule ya
msingi Sunzula ( A) wilayani Itilima mkoani Simiyu walazamika kutumia
tundu moja la choo na Walimu ambapo mahitaji ya choo ni matundu 28 hali
ambayo imesababisha kukwama kwa ufundishaji na ujifunzaji na pia inaweza
kusababisha milipuko ya magonjwa,hivyo jitihada zinahitajika kabla
shule hiyo
kufunguliwa januari mwakani .
Wakiongea na waandishi wa Habari walimu
wa shule hiyo wamesema kuwa baada ya choo cha wanafunzi kuanguka,
wanafunzi hao hawakuwa na njia mbadala ya kupata huduma hiyo na badala
yake walilazimika kwenda porini kabla ya kupewa choo cha walimu.
Wamesema kuwa baada ya kugundua kushuka
kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni hapo na chanzo kikiwa ni ukosefu wa
vyoo vya wanafunzi, walimu walilazimika kukigeuza choo cha chao chenye
tundu moja kutumika kwa wanafunzi wa jinsia zote.
Kwa upande wake Mbunge wa Itilima Njalu
Silanga ambaye yuko katika ziara jimboni mwake kujionea changamoto
zilizopo aliyepita shuleni hapo amesema yeye atamalizia choo hicho kwa
kujenga boma na kupaua lakini ameitaka jamii ya eneo hilo kuhakikisha
inamalizia kwa kuyafunika matundu hayo vizuri ili yeye amalizie.
HIKI NDIYO KISA CHA WALIMU KUSHIRIKI NA WANAFUNZI KATIKA VYOO HIVI
DAR ES SALAAM
Jumla ya Wanafumzi 7I0 wa shule ya
msingi Sunzula ( A) wilayani Itilima mkoani Simiyu walazamika kutumia
tundu moja la choo na Walimu ambapo mahitaji ya choo ni matundu 28 hali
ambayo imesababisha kukwama kwa ufundishaji na ujifunzaji na pia inaweza
kusababisha milipuko ya magonjwa,hivyo jitihada zinahitajika kabla
shule hiyo kufunguliwa januari mwakani .
Wakiongea na waandishi wa Habari walimu
wa shule hiyo wamesema kuwa baada ya choo cha wanafunzi kuanguka,
wanafunzi hao hawakuwa na njia mbadala ya kupata huduma hiyo na badala
yake walilazimika kwenda porini kabla ya kupewa choo cha walimu.
Wamesema kuwa baada ya kugundua kushuka
kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni hapo na chanzo kikiwa ni ukosefu wa
vyoo vya wanafunzi, walimu walilazimika kukigeuza choo cha chao chenye
tundu moja kutumika kwa wanafunzi wa jinsia zote.
Kwa upande wake Mbunge wa Itilima Njalu
Silanga ambaye yuko katika ziara jimboni mwake kujionea changamoto
zilizopo aliyepita shuleni hapo amesema yeye atamalizia choo hicho kwa
kujenga boma na kupaua lakini ameitaka jamii ya eneo hilo kuhakikisha
inamalizia kwa kuyafunika matundu hayo vizuri ili yeye amalizie.

0 comments :
Post a Comment