Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Babati Ambaye Alihusika na Kuibinafsisha Coco Beach Wakati Akiwa Kinondoni ASIMAMISHWA Kazi Kupisha Uchunguzi

@nkupamah blog

Katibu mkuu ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Bwana Jumanne Sagini amemsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara Mhandisi Mussa Natty ambaye (‪Pichani‬) kabla ya kuhamishiwa wilayani Babati alikua mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Bwana Sagini amefafanua kuwa pamoja na kusimamishwa kazi, Mhandisi Natty anapaswa kurudi katika halmashauri ya manispaa ya Kinondoni na kusubiri uchunguzi zaidi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Ametaja tuhuma hizo kuwa ni pamoja na usimamizi mbaya uliosababisha barabara za manispaa ya Kinondoni kujengwa chini ya kiwango na kutowachukulia hatua watendaji wa manispaa waliokua chini yake, ukosefu wa uadilifu katika ubinafsishaji wa eneo la ufukwe wa bahari la Coco Beach na malalamiko ya wananchi juu ya viwanja katika eneo la Kinondoni ulioambatana na usimamizi duni wa watumishi hasa wa sekta ya mipango miji na ardhi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment