Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael
Mhando akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Kituo cha
Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ambacho kitahusika na
kupokea na kujibu hoja za wadau mbalimbali zitakazowasilishwa katika
Mfuko kupitia Namba ya simu 0800 110063, barua pepe info@nhif.or.tz na
mawasiliano kwa njia ya mtandao (Mitandao ya kijamii na simu za
mkononi), uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es
salaam.Picha na Michuzi Blog
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani
Athumani (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa
uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ya
NHIF, uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es
salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael
Mhando akionyesha kipeperushi chenye namba ya mawasiliano ya moja kwa
moja na kituo hicho.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael
Mhando (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SoftNet Tech, Nuru Yakub
Othman wakishirikiana kuzindua rasmi Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa
Wateja (Call center) cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, uliofanyika
leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael
Mhando (kushoto) akimuangalia Ofisa Uanachama wa Kituo cha Mawasiliani
ya Huduma kwa wateja, Eva Mkwizu wakati akiwasiliana na wateja wa njia
ya simu. Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF), Beatus Chijumba
Baadhi ya Maofisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiendelea kutoa huduma katika kituo hicho.
Mmoja wa Maofisa wa mfuko huo Sabina akiendelea na kazi yake.








0 comments :
Post a Comment