Wednesday, December 2, 2015
 
@nkupamah blog
Tajiri huyo anayetambulika kwa jina la Nassoro Ahmed bin Slum anayemiliki kampuni ya Bin-slum Tyres Ltd, amejitokeza na kukiri kumiliki
 baadhi ya makontena yaliyokumbwa na kashfa hiyo lakini  amekana kosa 
lenye sura ya kukwepa kodi  akidai kuwa limefanywa na wakala wake.
“Wafanyabiashara
 hatuna mamlaka ya kulipa kodi moja kwa moja serikalini. Tunalipa kodi 
kupitia kwa wakala aliyechaguliwa na serikali. Mimi nilimlipa kazi 
wakala wangu ambaye nimekuwa nikifanya naye kazi kwa miaka 10,” Bin Slum ameliambia gazeti la Raia Mwema.
“Mara
 kwa mara huwa ananiletea nyaraka za malipo ya kodi lakini kwenye mzigo 
huu wa sasa  ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi, alinitangulizia 
mzigo na mimi nikamdai nyaraka. Yeye aliniambia ananiandalia faili,” alieleza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wote wanaohusika na kashfa hiyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua na kodi iliyokwepwa ilipwe.
Tayari watu 12 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia sakata hilo.



0 comments :
Post a Comment