Tasnia ya filamu nchini yachangia kutoa ajira na kuongeza pato la taifa

fl1 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akielezea namna sekta ya Filamu ilivyo piga hatua hapa nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Genofeva Matemu na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Fatma Salum.
fl2:
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo uliokuwa unahusu ukuaji wa sekta ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM
……………………………………………………………………………………………
Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Sekta ya filamu imekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa jumla ya ajira 732,681ikiwa ni mchango wake katika kutatua tatizo la ajira nchini kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Joyce Fissoo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Fissoo alifafanua kuwa idadi hiyo ya ajira zilizotolewa inajumuisha wataalamu wa filamu 944 na wadau wengine wasio wataalamu 731,737 ikilinganishwa na takwimu zilizotolewa na Shirika la Milki Bunifu Ulimwengini liliripoti kuwa mwaka 2007 tasnia ya filamu iliajiri watu 36.
‘Katika kipindi cha miaka ya 2000 utengenezaji wa filamu umebadilika kutoka ule wa awali wa kuburudisha na kuelimisha na kuwa biashara inayoingiza kipato na kutoa ajira katika jamii hivyo kuongeza kipato cha Taifa letu”. Alisema Fissoo
Aidha, kuanzia miaka ya 2000 sekta binafsi ilianza kutengeneza filamu hivyo filamu zilianza kufadhiliwa, kutengenezwa, kumilikiwa na kusambazwa kwa kiasi kikubwa na wadau na makampuni binafsi hivyo kupelekea ongezeko kubwa la makampuni ya uzalishaji na usambazaji kutoka kampuni 1 miaka ya 2000 hadi kufikia makampuni 250 mwaka 2015.
Tasnia hiyo imechangia kukuza uchumi wa nchi na ule wa mtu binafsi ambapo kwa mujibu wa Shirika la Milki Bunifu Ulimwenguni (WIPO) kwa mwaka wa 2007 ilichangia shilingi 2,134,860 na kufikia mwaka 2010 ilichangia shilingi 11,398,440, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 433.9.
Akizungumzia ukuaji huo wa tasnia ya filamu, Fissoo alisema kuwa ukuaji wa teknolojia umepelekea utumiaji wa vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu vilivyowekezwa na baadhi ya wadau vinavyopatikana kirahisi kama vile kamera za kisasa, na mashine za kufungashia kazi za filamu hivyo kupunguza gharama za uzalishaji wa filamu nchini.
Aidha, kumekua na uuzaji wa filamu kwa njia ya mtandao suala linalopanua wigo wa masoko na kuitangaza nchi kwa wepesi zaidi hivyo kupelekea umahususi wa mandhari ya Tanzania kutumika na watengenezaji wa ndani na makampuni ya nje yapatayo 169 kutengeneza filamu mbalimbali.
Tasnia ya filamu nchini imeendelea kukua na kushamiri kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo na wadau wa ndani ya nchi ikiwemo kuandaa, kuratibu  na kuendesha matamasha na Tuzo za Filamu za Tanzania (TAFA),Tamasha la Filamu la Bara la Ulaya, Tamasha la Filamu la Misri, Tamasha la Filamu la India, Tamasha la Filamu la Bara la Asia, Tamasha la Filamu la Brazil na Arusha African Film Festival.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment