Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya
Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu,
Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo
inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa kuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es
Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari
Polisi na Magereza.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu,
Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga mara baada ya kumuapisha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika
katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia
masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (katikati), mara baada ya Jaji
huyo kumuapisha Waziri Kitwanga kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya
Jeshi la Polisi na Magereza, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu
wa Waziri huyo, Nelson Kaminyoge.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akipandisha ngazi za kuingia Mahakama Kuu wakati
alipokuwa anaenda kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi
la Polisi na Magereza. Jaji Kiongozi wa Mahakama hiyo, Shabani Lila
alimuapisha Waziri Kitwanga Mahakamani hapo, jijini Dar es Salaam leo.
Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na
Magereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kulia) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Waziri Kitwanga kuapishwa na
Jaji huyo kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na
Magereza katika tukio lililofanyika Mahakamani hapo, jijini Dar es
Salaam leo.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu
nchini, Shabani Lila (katikati) akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) mara baada ya kumaliza kumuapisha kuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika
tukio lililofanyika Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo
inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Kushoto ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.


0 comments :
Post a Comment