Majira ya saa 10 na dakika 10
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo alifika katika mitambo ya
kuzalisha umeme wa gesi iliyoko Tegeta jijini Dar es Salaam
inachomilikiwa na Tanesco bila ya kutoa taarifa na kukuta wafanyakazi
pamoja na wahandisi wa kituo hicho cha umeme wakiendelea na kazi katika
mitambo hiyo.
Waziri Muhongo amekagua mitambo
hiyo leo na kubaini kuwa umeme uniti moja inatengenezwa kwa gharama ya
shilingi 90 na kuuzwa kwa wananchi kwa shilingi 180 ikiwa ni kiwango
kikubwa kwa mwananchi wa kawaida.
Pia Muhongo amesisitiza kuwa umeme unatakiwa kushuka bei ili kila mwananchi anufaike na nishati hiyo hapa nchini.
Waziri wa Nishati na Madini,
Sospeter Muhongo akipokea vifaa vya kuzuia kusikia sauti kuingia
masikioni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mitambo ya
Gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nishati na Madini,
Sospeter Muhongo akizungumza na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta
jijini Dar es Salaam, Mohamed Kisiwa mara baada waziri huyo kutembelea
mitambo ya umeme wa gesi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini,
Sospeter Muhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya
Tegeta, Mohamed Kisiwa mara baada ya waziri huyo kutembelea mitambo hiyo
bila kutoa taarifa na kuhoji baadhi ya matengenezo katika mitambo hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini,
Sospeter Muhongo akitembezwa na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta
Mohamed Kisiwa mara baada ya kutembelea mitambo ya Tegeta jijini Dar es
Salaam leo.
Baadhi ya Mitambo ya Gesi iliyotembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo leo jijini Dar es Salaam.








0 comments :
Post a Comment