Nkupamah media:
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kaimu
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma wa chama hicho, Hamad
Masoud, alidai CUF inatambua kwamba Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim
Jecha, anatekeleza
maagizo ya chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
maagizo ya chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema CUF inawataka wananchi wote wa Zanzibar, Tanzania na
jumuiya ya kimataifa kutambua kwamba Jecha ametoa taarifa ya uongo ili
kuendeleza upotoshaji alioanzisha kwa tamko lake la kufuta uchaguzi wa
Oktoba 25, mwaka jana na kuamuru kurudiwa uchaguzi huo.
Alisema CUF haitashiriki katika uchaguzi huo wa Machi 20, mwaka huu
na kuichia CCM iendelee kujitangazia ushindi wa urais, viti vyote 54
vya uwakilishi na viti vyote 111 vya udiwani.
Alisema CUF kitaendelea kusimamia maamuzi yake waliyafanya kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wa marudio katika nafasi zote.
Wakati huhuo, chama hicho, kimelitaka Jeshi la Polisi Zanzibar,
iwapo kweli lina kesi dhidi ya mwanaharakati wa CUF, Eddy Riyami,
limfikishe mahakamani haraka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake
na iwapo hawana kesi wamwachie huru.
Riyami anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu juzi kwa tuhuma za
kumtukana na kumkashifu Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, pamoja
na Jecha.


0 comments :
Post a Comment