Mgombea urais alievuliwa uanachama na ACT WAZALENDO Afunguka ..........Nitashinda urais uchaguzi wa maruidio Zanzibar'

Nkupamah media:

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Pamoja na chama chake kumpiga ‘stop’, mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT- Wazalendo, Khamis Iddi Lila, amesema amekuwa akiomba dua usiku na mchana aibuke mshindi katika uchaguzi mkuu wa
marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu visiwani humo na kwamba ina imani atashinda urais.
 Lila amesema ana matumaini makubwa ya chama chake kufikia malengo makubwa ya kisiasa visiwani humo baada ya kuibuka mvutano baina ya vyama vikuu vya CCM na CUF juu ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu na matokeo yake kufutwa na kusababisha CUF kususia uchaguzi huo wa marudio.
 
 Akizungumza mjini hapa mwishoni mwa wiki, Lila alisema mvutano wa CUF na CCM una tija kubwa kwa vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo kama wananchi watakubali kufanya mageuzi ya kukomesha ukiritimba wa kisiasa katika visiwa vya Zanzibar baina ya vyama hivyo viwili.
 
Alisema pamoja na viongozi wa chama chake kutangaza kumsimamisha uanachama kutokana na kushiriki uchaguzi huo wa marudio, bado anajitambua kuwa mgombea halali baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kueleza kuwa wagombea wote walioshiriki uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana ni wagombea halali katika uchaguzi wa marudio.
 
“Mvutano wa CUF na CCM una neema na tija kubwa kwa vyama vilivyobakia, ndiyo maaana naomba dua usiku na mchana nishinde urais wa Zanzibar,” aliongeza kusema Lila.
 
UONGOZI WAMKANA
Hata hivyo, uongozi wa chama ACT -Wazalendo Zanzibar haumtambui Lila kama mgombea wake na kama anashiriki uchaguzi huo atasimama kama mgombea binafsi.
 
Msimamo huo ulitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma Said Sanani, mjini Zanzibar jana, baada ya mgombea huyo kugoma kujitoa katika uchaguzi huo wa marudio.
 
Alidai Lila amefukuzwa uanachama wa ACT-Wazalendo kutoka na na kwenda kinyume na msimamo wa chama hicho wa kususia uchaguzi huo wa marudio.
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment