………………………………………
Serikali imesema kuwa italipa
kipaumbele suala la uhakiki wa mali za viongozi wa umma kwa kuiwezesha
Sekretarieti ya Maadili ya viongozi kufanya kazi zake kwa ukamilifu kwa
mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amesema hayoleo jijini Dar
es Salaam alipokutana na Kamati ya Kudumu yaBunge ya Utawala na Serikali
za Mitaa pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa imetembelea ofisi za Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa umma kujua majukumu, mafanikio na changamoto
zinazoikabili Taasisi hiyo ili wakifika bungeni waweze kuisemea.
“Suala la uhakiki wa rasilimali na
madeni ya viongozi tutahakikisha linapewa kipaumbele katika Awamu hii
ya tano ya uongozi,” amesema.
Kwa mujibu wa Waziri Kairuki,
Serikali itajitahidi kuongeza jitihada ili uhakiki wa rasilimali na
madeni ya viongozi wa Umma ufanyike, pamoja na kuiongezea Taasisi hiyo
bajeti ya kutosha.
Awali akitoa taarifa ya
utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe Salome Kaganda amesema viongozi wengi
wanarejesha fomu za raslimali na madeni, ila wapo wachache wanaoshindwa
kurejesha fomu hizo.
Amesema, “Tangu mwaka 2005/06 hadi
mwaka 2014/15 tumesambaza fomu 78,786, lakini fomu zilizorejeshwa ni
60,948 ambazo ni sawa na asilimia 77 ya fomu zote zilizosambazwa.”
Aidha Kamishna huyo
amewaambiawajumbe wa kamati hiyo ya Bunge kuwa tangu mwaka 2013 hadi
2015 Sekretarieti yake haikufanya uhakiki wa rasilimali na madeni kwa
viongozi wa umma kutokana na ufinyu wa bajeti.
Kwa upande wao baadhi ya Wajumbe
wa kamati wamesema kuwa wataishauri serikali kuiongezea Sekretarieti
bajeti iliiweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sharia.
Pia wamependekeza kufanyiwa
maboresho Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 ili
iwe na nguvu zaidi na kuwaruhusu kuwafikisha mahakamani viongozi
wanaokiuka sharia hiyo.
Sekretarieti ya Maadil ilianza
kufanya kazi rasmi mwezi Julai, 1996 ikiwa na jukumu la msingi la
kujenga na kukuza uadilifu miongoni mwa Viongozi wa Umma kwa kusimamia
utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma Na 13 ya
mwaka 1995.
0 comments :
Post a Comment