Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto)
akikisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali
ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata
kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto)
akibadilishana hati ya makubaliano walizosaini na Serikali ya Japan
utakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na
Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini
Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya
makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini
Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6
ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
Balozi
wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati
ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam
ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na
Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao wakati wa hafla ya
kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya
Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi
Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
(Na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan
itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na
Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika
kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.
Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada
huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha
masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira
nchini.
Mkataba wa pili unahusu masuala
ya kiufundi yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba
uliosainiwa Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika,
kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi
ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza
miradi ya maendeleo nchini.
Aidha, makubaliano hayo yatasaidia
kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele
cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya
wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa
nchini Tanzania.
Katibu Mkuu Dkt. Likwelile
ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika
kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo
Watanzania.
Naye Balozi wa Japan nchini
Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani
kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza
maendeleo ya uchumi na kijamii.
Balozi Yoshida amesema kuwa
Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na
Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri
yanayovutia wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania.
Adha amesema kuwa Japan itaendelea
kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii
jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya
vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500.
0 comments :
Post a Comment