Muogeleaji Marin de Villard wa Tanzania akishindana katika staili ya backstroke kwenye mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini.
Muogeleaji
wa Tanzania Celina Itatiro akionyesha ufundi wake katika staili ya
backstroke kwenye mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini.
Muogeleaji
wa Tanzania, Adil Bharmal akiwa katika staili ya breaststroke kwenye
mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini.
Nyuso
za furaha: Meneja wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS), Inviolata
Itatiro akiwa na makocha, Alex Mwaipasi (kushoto) na Michael Livingstone
mara baada ya ushindi wa medali tatu katika mashindano ya kuogelea ya
Kimataifa ya Afrika Kusini.
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Nyota ya Tanzania katika mchezo
wa kuogelea imeanza kung’ara baada ya kupata medali tatu katika
mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini yanayondelea katika
mji wa Johannesburg.
Walioshinda medali katika
mashindano hayo ni, Josephine Oosterhuis, Isabella Kortland na
Jacqueline Kortland katika mashindano hayo ambayo yanashirikisha
waogeleaji zaidi ya 750 kutoka nchi mbalimbali kusini mwa Afrika.
Mbali ya Tanzania na wenyeji,
Afrika Kusini, mashindano hayo pia yalishirikisha timu kutoka Zimbabwe,
Msumbiji, Angola, na Namibia. Josephine alishinda medali ya dhahabu
katika fainali ya mita 100 breaststroke kwa kutumia muda wa 1.21.79 huku
Jacqueline alishinda medali ya shaba kwa kushika nafasi ya tatu kwa
kutumia muda wa 1.22.91.
Nafasi ya pili ikikwenda kwa
Deane Toerien wa Afrika Kusini aliyetumia muda wa 1.22.70 na kutwaa
medali ya fedha. Isabella Kortland alishinda medali ya dhahabu kwenye
mashindano ya mita 50 katika staili ya backstrokes kwa kutumia muda wa
33.25 kuwashinda Georgy Turner na Zantia Bainabridge wa Afrika Kusini
ambao walifungana kwa kutumua muda wa 33.84 kila mmoja.
Waogeleaji Celina Itatiro
hakuweza kutwaa medali pamoja na kumaliza akiwa wa tisa kwa kutumia muda
wa 1.29.26 katika mita 100 butterfly, Marin de Villard alimaliza wa
tisa katika staili ya backstroke kwa kutumia muda wa 37.43.
“Tumefanya vizuri sana, si
unajua mashindano haya ni magumu kutokana na ushindani uliopo, Afrika
Kusini na nchi nyingine inatumia kutafuta waogeleaji wao ambao
watakwenda kushindana katika mashindano ya Cana na wameleta waogeleaji
wengi, sisi tumeleta 15 na mpaka sasa tuna medali 3, ni mafanikio,”
alisema meneja wa timu hiyo Inviolata Itatiro.
Kocha Alex Mwaipasi alisema kuwa
wamefurahishwa na matokeo hayo na wanaamini kuwa wakiendelea na msimamo
wao wa kushiriki mashindano mengi ya kimataifa, basi watafika mbali
sana ndani ya miaka mitano au kumi.
“Mbali ya medali, hapa
waogeleaji wanasaka nafasi ya Cana, baadhi ya waogeaji wetu ndiyo kwanza
wanaogelea katika bwawa la mita 50, wengine mara ya kwanza, hivyo kuna
changamoto,” alisema Mwaipasi.
Kocha Michael Livingstone
aliwashukuru wazazi wa waogeleaji kwa kufanikisha safari hii na kuifanya
Tanzania kuingia katika chati ya mchezo wa kuogelea. “Wazazi
wamejitahidi kwa kweli, wengine wameshindwa na wengine wameambatana na
watoto wao kuja hapa kwa ajili ya kuitangaza Tanzania, tumefanikiwa,”
alisema Michael.
0 comments :
Post a Comment