TRUMP NA CLINTON WAONGOZA JUMANNE KUU

Nkupamah media:

Clinton
Clinton ameshinda majimbo matano
Mgombea wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump wamechukua uongozi wa mapema katika mchujo wa kuteua wagombea urais Marekani katika vyama vyao.
Wagombea wote wawili wameshinda majimbo ya Alabama, Georgia, Tennessee na Virginia.
Bw Trump hata hivyo ameshindwa na Seneta Ted Cruz majimbo ya Texas na Oklahoma.
Mgombea wa Democratic Bernie Sanders naye ameshinda kwake nyumbani katika jimbo la Vermont na pia katika jimbo la Oklahoma.
Trump
Donald Trump anaongoza chama cha Republican
Mchujo wa Jumanne Kuu hushuhudia majimbo 11 yakifanya mchujo kwa pamoja huku maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe 8 Novemba yakiendelea kushika kasi.
MOJA KWA MOJA: Mchujo wa Jumanne Kuu Marekani
Bi Hillary Clinton, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, pamoja na mfanyabiashara tajiri kutoka New York Donald Trump walipigiwa upatu kushinda majimbo mengi Jumanne Kuu.
Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na Texas, naye Bw Trump akashinda Massachusetts.
Utafiti wa maoni ya paada ya kura unaonyesha Trump na gavana wa Ohio John Kasich wakikabiliana vikali katika mchujo wa chama cha Republican jimbo la Vermont.
Bi Clinton na Bw Sanders pia wanakabiliana vikali katika jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa Marekani.
Matokeo kutoka majimbo yaliyosalia yanatarajiwa kutolea katika saa chache zijazo.BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment