Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza katika kikao cha Mapitio ya
Rasimu ya Bajeti ya Wizara yake ya Mwaka 2016/17 kwa upande wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo,
kilijumuisha Viongozi Wakuu wa Taasisi hizo pamoja na Wakuu wa Idara wa
Wizara hiyo. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba
Yahya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kushoto) akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) wakati alipokuwa anatoa taarifa yake
katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Idara
ya Uhamiaji kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo,
jijini Dar es Salaam leo. Kikao hicho kilijumuisha Viongozi Wakuu wa
Uhamiaji na Wakuu wa Idara ya Wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akiwafafanulia jambo Viongozi Wakuu wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji na Wakuu wa Idara ya Wizara yake katika kikao cha
Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Jeshi hilo
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es
Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali
Projest Rwegasira. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Balozi Simba Yahya, na wa tatu kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Rogatius Kipali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (wapili kulia) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Idara
ya Uhamiaji katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka
2016/17 ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, pia kilihudhuriwa na
Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira, na wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akifuatiwa na Mrakibu Mwandamizi
wa Idara ya Uhamiaji, Joseph Mtenga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments :
Post a Comment