Droo ya
Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup),
inatarajiwa kufanyika kesho Jumanne saa 3 usiku moja kwa moja (live)
kupitia kituo cha luninga cha AzamTwo.
Hatua ya
Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itafanyika live katika kituo
cha AzamTwo, ambao kupitia Azamtv ndio wadhamini wa wakuu wa michuano
hiyo iliyoibua msisimiko wa mpira wa miguu na kushirikisha timu nyingi
zaidi nchini.
Baada ya
timu za Azam FC, Mwadui FC, na Yanga SC kukata tiketi ya kucheza Nusu
Fainali, mshindi wa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Coastal Union
utakaochezwa leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam atungana na
timu hizo tatu kwenye droo ya kesho.
Michuano
ya Kombe la Shirikisho iliyoanza kwa kushirikisha timu 64 mwishoni mwa
mwaka jana, imefikia hatua hatua ya nusu fainali, baada ya Azam FC
kuindoa Prisons (3-1), Mwadui FC kuiondosha Geita Gold (3-0) na Yanga SC
kuwaondoa Ndanda FC kwa mabao (2-1).
Mshindi
wa Kombe la Shirikisho (ASFC) msimu huu, ataiwakilisha Tanzania mwaka
2017 katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC).(P.T
0 comments :
Post a Comment