Baada
ya jana Feb. 11 Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima
kuachiwa na Polisi baada ya mahojiano yaliyodumu toka Alhamisi kituo cha
Polisi kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya, leo
February 12 2017 akiwa kwenye Ibada kanisani kwake amesimulia.
"Nilienda
moja kwa moja kwa Kamanda Sirro, nikamkuta na Manji, wakasema wewe na
Manji tunakwenda kuwapima kwa mkemia mkuu wa Serikali, wale watu
waliokuwa wanapima walikuwa wanapima kwa uwazi kabisa, wakapima vitu
vyote majibu hamna chochote.
“Waliposema
twende tukapime nilikua tayari, na mimi nilisema ndani yangu hata
ukiona Pombe andika umeona dawa za kulevya, nikasema mimi sina tatizo
twendeni nyumbani kwangu na mkikuta hata sigara andikeni ni dawa za
kulevya, wakasachi na hawakukuta kitu”
==>Msikilize hapo chini akiongea
0 comments :
Post a Comment