Amzidi utajiri Bill Gates kwa saa nne

  • Tukio hilo limetokea nchini Marekani na kuvuta wengi kwenye mitandao ya kijamii.  
Tajiri Jeff Bezos ameshikilia nafasi ya kwanza kwa utajiri duniani kwa saa nne na baadaye kushuka hadi ya pili.
Bezos anayemiliki mtandao wa Amazon, utajiri wake ulipanda na kufikia Dola 92.3 bilioni za Marekani akimshinda Bill Gates mwenye utajiri wa Dola 90.8 bilioni.
Tajiri Bezos alishika nafasi ya kwanza Alhamisi, Julai 27 baada ya mauzo ya hisa ya kampuni ya Amazon kupanda kwa asilimia tatu.
Hata hivyo, alishuka hadi nafasi ya pili baada ya mauzo ya hisa ya kampuni hiyo kushuka na kufikia asilimia 0.7.
Hatua hiyo  ilimfanya kushika nafasi ya pili kwa utajiri wa Dola 89.3 bilioni na Gates akiwa na Dola 90.7 bilioni.
Mwisho
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment