Kaimu rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania, Wallace Karia atalazimika kupimwa vinasaba (DNA) ili kuthibitisha uraia wake, utakaotoa mustakabali wa mbio zake za kuwania urais katika uchaguzi wa shirikisho hilo.
Hatua hiyo ni kwa mujibu wa vyanzo vya ndani vya mamlaka mbalimbali zinazohusika na suala hilo ikiwa ni siku chache baada ya Karia kuhojiwa na idara ya uhamiaji, mahojiano ambayo bado hayajatoa suluhu ya utata huo.
Kwa upande wa Idara ya Uhamiaji Kitengo cha uraia imethibisha kuendelea na uchunguzi wa uhalali wa uraia wa mgombea huyo ambapo msemaji wake Ally Mtanda ameiambia Mshikemshike Viwanjani katika mahojiano maalum kwamba wapo katika hatua za mwisho na siku si nyingi watatoa majibu yao.
Kwa mujibu wa Mtanda, Karia amesema yeye ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa na pia mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Tanzania licha ya mzazi wake mwingine kuwa na asili ya Somalia.
Kwa maelezo hayo, ni dhahiri kwamba zoezi la vipimo vya vinasaba ndilo litakalotoa muafaka wa sakata hilo.
Karia ni kati ya wagombea sita waliopitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kugombea urais, wengine wakiwa ni Ally Mayay, Wakili Imani Madega, Frederick Mwakalebela, Emmanuel Kimbe na Shijja Richard
0 comments :
Post a Comment