Timu ya taifa ya riadha ya Tanzania itakayoshiriki mashindano ya riadha ya dunia yanayoanza wiki hii jijini London Uingereza imeagwa rasmi leo na kukabidhiwa rasmi bendera ya Taifa.
Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji nane imeagwa katika hafla iliyohudhuriwa na waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dkt. Harisson Mwakyembe ambaye amewasisitiza wanariadha hao kuongeza bidii ili waweze kuiletea sifa nchi.
Akitoa siri kwa wanariadha hao kurudi na medali, Mwakyembe amesema kuna siri tatu pekee ambazo ni pamoja na mazoezi ya nguvu yasiyotegemea dawa za kuongeza nguvu wala uchawi.
Siri nyingine ni wachezaji kuwa na ari ya ushindi na siri ya tatu ni mapenzi na uzalendo kwa taifa, mambo ambayo amesema kuwa anayaona kwenye nyuso za wanariadha hao
Kwenye mashindano hayo yanayotarajia kuanza Agosti 4 na kuendelea kwa takriban siku 10, wanariadha watano kutoka Tanzania watashiriki mbio za kilomita 42 na watatu mbio fupi
0 comments :
Post a Comment