Rais Mstaafu kukamatwa na polisi kwa tuhuma za rushwa

Polisi nchini Malawi wametoa kibali cha kukamatwa kwa rais wa zamani Joyce Banda kuhusiana na sakata ya ulaji rushwa inayofahamika sana kama Cashgate wakati wa utawala wake.
Joyce Banda alikuwa rais kati ya 2012 na 2014
Polisi wamesema wamepata ushahidi wa kuaminika kuhusiana na sakata hiyo ya $250m (£190m).
Kashfa hiyo „inaibua uwezekano kwamba huenda rais huyo wa zamani alitenda makosa yanayohusiana na kutumia vibaya mamlaka na utakatishaji wa fedha.
Bi Banda yuko nje ya nchi na polisi wan chi hiyo wamesema wataomba msaada kutoka kwa polisi wa kimataifa Interpol kuhakikisha anarejea nchini humo kujibu mashtaka Cashgate ndiyo sakata kubwa zaidi ya ufisadi kuwahi kutokea katika historia ya Malawi.
Sakata hiyo inahusisha kuporwa kwa fedha za umma wakati wa utawala wa Bi Banda.
Rais huyo wa zamani hajazungumzia tuhuma hizo zilizotolewa dhidi yake.
Chanzo:BBC Swahili
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment