TOKYO,Japan
MACHAMPION wa ligi ya Mabingwa Ulaya,Fc
Barcelona wamefanikiwa kutwaa taji la klabu bingwa ya dunia ,mara baada
ya kuwafunga mabingwa wa bara la Amerika kusini River Plate kwa jumla ya
goli 3-0

Katika
mchezo huo uliomalizika hivi punde,magoli ya Fc Barcelona
yalipatikanika kuanzia katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 36
ambapo Lionel Messi alimalizia pasi aliyochongewa na Neymar na
kuiandikia Barcelona goli la kwanza.

Mchezo
huo ambao ulihusisha ufundi mwingi kwa kila timu,ulishuhudia kipindi
cha kwanza kikimalizika kwa Fc Barcelona kuwa mbele kwa jumla la goli
2,ambapo goli la pili la Barcelona lilifungwa na Luis Suarez katika
dakika ya 49 ya mchezo huo akimalizia pasi kutoka kwa Neymar.

Kipindi
cha pili kilinza huku kila timu ikijitahidi kujizatiti katika kusaka
magoli,lakini walikuwa ni Barcelona kupitia kwa Luis Suarez aliyeandika
goli la tano kwa upande wake katika mashindano hayo na goli la tatu kwa
timu yake katika dakika ya 68 ya mchezo akimaliza pasi murua ya Neymar.

Kwa
matokeo hayo Barcelona wanajihakikishia kombe la tano kwa mwaka
huu,ambapo mapema mwezi wa nne walitwaa taji la ligi kuu Hispania,kisha
wakatwaa kombe la mfalme,likafuatiwa na taji la ligi ya mabingwa ulaya
na taji la super cup la michuano ya klabu bingwa Ulaya
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment