Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.
Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.
“Nadhani sasa unaelewa
niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora
zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo inahitaji
udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka, nimefurahi sana,” Dk. Slaa ameliambia gazeti la Raia Mwema.
Amesema kuwa Bunge linatakiwa
kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili usivuke mipaka lakini
limuunge mkono kwa hatua anazochukua.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa
amemshauri Rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) na kuifumua.
“Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.
0 comments :
Post a Comment