Naibu Waziri Wizara ya Nishati
na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akimsikiliza Naibu Mkurugenzi
Mtendaji Tanesco Bw.Decklan Mhaiki alipokuwa akimwonyesha mradi wa
Kinyerezi I mara baada ya kuwasili katika kituo cha kuzalisha umeme kwa
kutumia gesi eneo la
Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi TANESCO Mhandisi
Simon Jalima (wa pili kushoto) akimwonyesha Naibu Waziri Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kulia) moja ya mtambo
unaopokea gesi kutoka mtwara na kuisambaza mpaka kituo cha Ubungo
alipofanya ziara ya kuona maendeleo ya mradi huo leo katika eneo la
mradi Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Naibu
Mkurugenzi Mtendaji Tanesco Bw. Decklan Mhaiki.
Meneja Mradi TANESCO Mhandisi
Simon Jalima (wa pili kushoto) akimtembeza Naibu Waziri Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kulia) kumwonyesha
mitambo mbalimbali ya uzalishaji wa umeme uliyopo katika kituo hicho cha
Kinyerezi I, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wataalamu wa
kuendesha mitambo inayosambaza nishati ya umeme uliyozalishwa kwa
kutumia gesi (Shift Supervisor) Bw. Mohamed Lanzi akimwonyesha Naibu
Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza
kulia) mtambo wa usambazaji wa umeme wa Morogoro unaotokea Kinyerezi I
namna wanavyouendesha.
Meneja Mradi wa Kinyerezi
Extension kutoka Kampuni ya Sumitomo Japan Bw. Shoji Watanabe akimweleza
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani ni kwa
muda gani mradi huo utakamilika mara baada ya kupewa mkataba wa kuanza
kazi hiyo, leo Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati
na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kulia) akitoa maagizo kwa
Meneja Mradi wa Kinyerezi Extension kutoka Kampuni ya Sumitomo Japan
Bw. Shoji Watanabe (wa kwanza kushoto) alipokuwa akigua eneo la mradi
huo leo Kinyerezi jijini Dar es Salaam, (wa pili kulia) ni Naibu
Mkurugenzi Mtendaji Tanesco Bw. Decklan Mhaiki.
Na Anitha Jonas –MAELEZO
Wizara ya Nishati na Madini
imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha
uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kinyerezi I na Kinyerezi II
unakamilika ifikapo mwezi Februari 2016 na kuanza kufanya uzalishaji
ilikuongeza kiasi cha nishati ya umeme kufikia zaidi ya Megawati 100.
Agizo hilo lilitolewa leo na Naibu
Waziri, Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani alipofanya
ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Gesi
cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam,hii ni baada ya kuelezwa kuwa kituo
hicho kwa sasa kinazalisha 70 Megawati za umeme ambaohautoshelezi kwa
matumizi ya watanzania.
“Watanzania wamechoshwa na mgao wa
umeme na wanaimani kubwa na uzalishaji wa kituo hiki cha kuzalisha
umeme kwa kutumia gesi hivyo wanatarajia umeme wa uhakika katika kufanya
shughuli mbalimbali za uzalishaji na kujipatia kipato”,alisema
Dkt.Kalemani.
Hata hivyo Dkt. Kalemani
aliwapongeza watendaji wa TANESCO na wakandarasi wanaosimamia uendeshaji
wa mitambo hiyo ya uzalishaji huku akiwasihii waongeze jitihada za
dhati kwani watanzania bado hawaridhishwi na kiasi cha umeme
kinachozalishwa kwa sasa.
Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara
ya Nishati na Madini Mhandisi Omari Chambo alisema kuna mradi mpya
uitwao Kinyerezi Extension unakaribia kuanzishwa hivi karibuni ambao
utazalisha Megawati 345 za umeme na kupitia mradi huu uzalishaji wa
umeme utaongezeka kwa kiasi kubwa.
“Tutajitahidi kwa sasa umeme
usikatike mara kwa mara na jitihada za kusafisha mitambo miwili ya phase
I na Phase II inafanyika na itakapokamilika tunatarajia kuzalisha zaidi
ya Megawati 140 za umeme na usafishaji wake unatarajiwa kukamilika
mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu”,alisema Mhandisi Chambo.
Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji
TANESCO Bw.Decklan Mhaiki alisema mradi wa Kinyerezi Extension ambao
utagharimu jumla ya kiasi cha Dola Milioni 340 unatarajia kuanza hivi
karibuni mara baada ya kukamilika kwa Mkataba na malipo ya 15% kwa
mkandarasi.
Pamoja na hayo wizara ya Nishati
na Madini imetoa angalizo kwa watendaji wote wanaozalisha umeme kwa
kutumia maji walinde vyanzo vya maji na kuacha kutumia maji hayo kwa
matumizi mengine kama ya kilimo.
Uzalishaji wa umeme kwa kutumia
Nishati ya Gesi utasaidia kupunguza gharama za watumiaji wa umeme pamoja
na kushusha gharama za uzalishaji.
0 comments :
Post a Comment