EXCLUSSIVE: PRODYUZA WA NAGHARIMIA, SUBIRA, CHEKECHA AMEAMBULIA MILIONI 5 MWAKA MZIMA

@nkupamah blog

DAR ES SALAAM


Kufuatia uvumi ambao ulienea kuwa Abby Daddy wa Chaiderz Records ambaye ni Prodyuza wa hits ya Chekecha cheketua, Subira ya Kasim Mganga, Nagharamia ya Alikiba ft Christian Bella, Unanimaliza ya Matonya, mkungu wa ndizi ya Q Chief ftTID na ngoma zingine za Abdu Kiba ft Ruby na Malaika ambazo zimefanya vizuri mtaani hajafaidika na kazi kwa mwaka 2015, @nkupamah blog ilifanya jitihada za kumtafuta kutaka kujua jambo hilo lina ukweli kiasi gani

Katika mazungumzo na mtembezi.com Prodyuza huyo ameweka wazi kuwa kwa mwaka huu licha ya kufanya kazi nyingi na nzuri ameambulia shilingi milioni Tano ambazo kiuhalisia ni sawa na bure ukilinganisha na kazi kubwa aliyofanya mwaka huu.ABBY DADDY

Hata hiyvo ameongeza kuwa kiasi hicho cha fedha hakikulipwa kwa pamoja ni baada ya kufanya majumuisho mabayo ameuambia mtandao huu kuwa huenda zikafikia kias hicho, na fedha hizo zilikuwa zinalipwa na msanii anapo jisikia mwenyewe na wengine haajamlipa mpaka leo

Aidha sababu kubwa amedai kuwa, kwa mwaka huu alitazama (Focus) kujulikana na kulikuza jina lake zaidi kuliko kutengeneza fedha lakini kwa mwakani amesema amejipanga kuweka mikataba ya malipo na wasanii ambao wata taka kufanya kazi na studio yake ya “Chaiderz Records”ABBY DADDY

Licha ya kufanya hivyo kwa mwaka huu Prodyuza huyo amesema changamoto kubwa ambayo alikumbana nayo ilikuwa ni msanii kuotofika studio kwa muda na siku waliopangiana

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment