LONDON,England
MIKIKIMIKIKI ya ligi kuu soka
Uingereza maarufu kama EPL inazidi kushika kasi katika ligi hiyo abayo
inahusudiwa na mamilioni ya mashabiki wa soka duniani,hii inatokana na
ugumu wa ligi hiyo ambao unazidisha burudani kila uchwao.
Gumzo kubwa katika soka hivi sasa ni juu
ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa Chelsea,Jose Mourinho ,kufanya
vibaya kwa Man United katika michuano ya klabu bingwa pamoja na maajabu
yanayofanwa na timu ya Leicester City.
Yote tisa kumi ni juu ya namna ambavyo
mshambulijai hatari wa Leicester City Jamie Vardy anavyozidi ‘kutumbua
majipu’ ya timu pinzani kila anavyopata nafasi ya kucheza katika kikosi
chake
.
Vardy ambaye hadi sasa anaongoza katika
msimamo wa ligi kuu akiwa na magoli 12 akifuatiwa kwa mbali na mchezaji
mwenzake katika timu moja Riyad Mahrez mwenye magoli 7, amekuwa moto wa
kuotea mbali hali inayosababisha klabu kubwa mbalimbali kutaka huduma
yake katika kipindi hiki cha kuelekea katika dirisha dogo la usajili
mwezi january.
Mathalani
klabu kama Chelsea,Man United,Liverpool na Real Madrid ni miongoni mwa
klabu kubwa ambazo zimetajwa kufukuzia saini ya mchezaji huyo wa
kiamtaifa wa Uingereza.
Pamoja na makali hayo pindi awapo
dimbani,Jamie amesema kuwa anayechagiza yeye kuwa katika kiwango cha
kutisha ni pamoja na wachezaji wenzake na mbinu toka kwa kocha wake
Claudio Reneir.
CHIMBUKO LA JAMIE RICHARD VARDY.
Mchezaji huyu ambaye amejumuishwa katika
kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza mara 4 tu katika historia
yake,amezaliwa mwaka 1987 katika mji wa Sheffield nchini Uingereza
Akiwa na miaka sita tu,Jamie alijiunga
na timu ya mtaani kwake inayoitwa Sheffield Wednesday ambapo alicheza
katika timu hiyo kama mshambuliaji hadi mwaka 2002,mwaka uliofuata Jamie
alijiunga na Stocksbridge Park Steel ambapo hii ikawa klabu yake ya
kwanza katika soka rasmi la ajira tofauti na kule alikotoka ambako
alicheza soka la riadhaa.
Akiwa katika timu hiyo,Jamie alicheza
jumla ya michezo 107 na kufanikiwa kupachika kimiani jumla ya magoli 66
hali iliyomfanya awe miongoni mwa washambuliaji hatari na wa kutumainiwa
na klabu yake.
Cheche za Jamie ziliifanya klabu hiyo
kumpandisha hadi timu ya wakubwa ambapo alidumu na timu hiyo hadi msimu
wa 2010/11 ambapo alisajiliwa na klabu ya Fc Halifax Town ambapo akiwa
hapo alicheza jumla ya michezo 37 na kufunga jumla ya magoli 27.
Akiwa na klabu hiyo Jamie alitunukiwa
tuzo ya mchezaji bora wa klabu hali iliyozidi kumpa sifa na kumfanya
azidi kuzifutia klabu nyingine mbalimbali.
Msimu wa 2011/12 alisajiliwa na klabu ya
Fleetwood Town ambapo akiwa hapo alicherza jumla ya michezo 36 na
kufunga magoli 31 wasatani wa goli moja katika kila mechi .
Msimu huo ukiwa umemalizika kwa Jamie
kuwa mfungaji bora katika klabu yake,klabu ya Leicester City ilivutiwa
na huduma zake na kuamua kumsajili kwa dau la pauni milioni 1 katika
mkataba wa miaka 3 ambao unakamilika mwishoni mwa msimu huu.
Akiwa na timu hiyo kabla ya hata kupanda
kucheza ligi kuu,alionyesha ni jinsi gani klabu hiyo alilamba
dume,kwani katika mechi 113 ambazo ameanza amefunga jumla ya magoli 40.
Jamie akiwa na Leicester City
amefanikiwa kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na mshambuliaji wa
zamani wa Man United,Ruud Van Nistelrooy ya kufunga katika michezo 11
mfululizo kitu ambacho hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kukifanya.
KUICHEZEA TIMU YA TAIFA.
Kwa mara ya kwanza Jamie aliitwa
kuichezea timu yake ya taifa tarehe 21 mwezi wa tano mwaka huu katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland,kabla ya kuitwa tena
katika kikosi cha timu hiyo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za
michuano ya Euro 2016 dhidi ya Slovenia.
Aidha hadi kufikia sasa mchezaji huyu
hajafanikiwa kufunga goli hata moja katika timu yake ya taifa.pia
aliitwa katika mechi dhidi ya San Marino na Switzeland.
STAILI YAKE YA MCHEZO.
Wachambuzi wengi wa soka na makocha wa
timu mbalimbali wanafananisha uchezaji wa Jamie Vardy na mchezaji wa
zamani wa England Salvatore Schillaci ambaye aliichezea Uingereza katika
michuano ya kombe la dunia mwaka 1990.
Hata hivyo imeelezwa kuwa Jamie hupenda
zaidi kucheza soka la nguvu na kushambulia kwa kasi huku akitumia
maarifa katika kuwatoka wachezaji na mabeki wa timu pinzani.
MAISHA BINAFSI YA JAMIE VARDY.
Inaelezwa kuwa Jamie ni moja kati ya
wachezaji ambao hawana matukio ya kuhuzunisha,japo taarifa za hivi
karibuni zinasema kuwa alihusika katika kutoa maneno ya kibaguzi dhidi
ya raia mmoja wa Japan ambapo amwita jina la ‘jap’ ambalo lilitafsiriwa
kama ni ubaguzi kwa mtu huyo.
Kufuatia kitendo hiko klabu yake
ilimlima faini na kumpa adhabu nyingine ambazo zilitokan an kukiri kutoa
kauli hiyo kwa mjapani huyo wakati akiwa klabu yeye na rafiki yake
Mbali na hayo mchezaji huyo ambaye kwa
sasa anapokea mshahara wa wiki wa pauni 45,000,kabla ya kujihusisha moja
kwa moja na soka la ushindabi,anaripotiwa kuwa amewahi kuhudhuria
mafunzo ya uuguzi mwaka 2007
Aidha mapema hivi karibuni Jamie
alifungua academy aliyoipa jina la V9 ambayo itakuwa na lenmgo la
kuwakutanisha wachezaji wote ambao wanaanza soka bila ya kuwa ndani ya
mfumo wa academy kama ambavyo yeye alianza soka la mitaani
MAFANIKIO BINAFSI
Moja
kati ya mafaniko aliyoyapa ni pamoja na kuibuka mfungaji bora katika
ligi daraja ya pili Championship wakati akiichezea klabu yake ya sasa
kabla haijapanda ligi kuu,lakini mafanikio yake ya hivi karibuni ni
pamoja na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi novembar ya ligi kuu
soka UIngereza huku akiwabwaga washindani wake mahiri kama Harry Kane


0 comments :
Post a Comment