Muhimbili Yafunga CT-Scan Nyingine


UM9 
Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH)  inafunga mashine nyingine ya CT- Scan ambayo inategemewa kuanza kutoa huduma kesho mchana.
“Hivyo kufikia jumatatu ijayo  Hospitali hiyo itakua na mashine mbili za CT-Scan  ambazo zitakua zinafanya kazi  hatua ambayo itaboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wagonjwa ambao wanatakiwa kupimwa kwa kutumia mashine hiyo,” amesema Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Watoto na Wazee  Ummy Mwalimu.
 
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Watoto na Wazee Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo wakati alipotembelea mashine   za CT-Scan na MRI katika hospitali hiyo.
 
Pamoja na mambo mengine Waziri  huyo  ameshauri ripoti za wagonjwa wanapimwa kwa kwa kutumia  mashine hizo zitolewe haraka ili kuwapunguzia gharama za kukaa muda mrefu wagonjwa wanaotoka katika mikoa mingine. 
Akizungumzia kuhusu mashine ya CT-Scan na MRI ambazo zimeharibika Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MHN Profesa Lawrence Mseru amesema juhudi za kutengeneza mashine hizo zinafanyika na kwamba kifaa cha CT- Scan kilichoharibika kitaingia leo usiku wakati  Spea  ya MRI  imeshawasili na matengenezo yanaendelea. 
Mashine ya  CT-Scan  hupima wastani wa wagonjwa  40 hadi  60 kwa  saa 24  wakati MRI  hupima wagonjwa 20 kwa siku.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment