Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa Bw. Michael Muhando akikabidhi vifaa tiba kama
vile Ultra Sound, Incubator, Mashine ya dawa za Usingizi ,Vitanda vya
Kujifungulia na Kadhalika kwa Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya mkoa wa
Singida Pendaeli Maasay leo
mkoani humo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa Bw. Michael Muhando akiangalia vifaa tiba
mbalimbali vilivyotolewa na mfuko huo kwa hospitali ya Mkoa wa Singida.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa Bw. Michael Muhando akimuonyesha vifaa tiba
vilivyokabidhiwa Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya mkoa wa Singida Dkt.
Ernest Mugeta na kushoto ni Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya mkoa wa
Singida Pendaeli Maasay
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa Bw. Michael Muhando akimuonyesha vifaa tiba
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya mkoa wa Singida Dkt. Ernest Mugeta.
…………………………………………………………………………………..
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bwana Michael Mhando ameelezea
kuridhishwa na matumizi ya mkopo uliotolewa kwa Hospitali ya mkao wa
Singida.
Hospitali hiyo ilichukua mkopo wa
Shilingi Milioni Mia Tano kutoka NHIF kwa ajili ya Ununuzi wa vifaa
Tiba vya hospitali hiyo. Akizungumza baada ya kukagua vifaa hivyo Bwana
Mhando baada ya amesema ameridhiswa na matumizi ya mkopo huo kwani
umefanya kazi iliyokusudiwa.
Amesema NHIF itaendelea
kushirikiana na uongozi wa mkoa huo ili kuboresha huduma za matibabu kwa
wanachama wa NHIF na wananchi kwa ujumla.
Aidha amewahimiza watoa huduma
wengine kuendelea kuchukua mikopo ili kuboresha huduma ktk vituo vyao
vya matibabu. Hivi sasa Mfuko huo umeanza pia kutoa mikopo ya dawa ili
kukabiiliana na uhaba wa dawa ktk vituo vya matibabu.


0 comments :
Post a Comment