Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin Eralp kisalimia na
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia
Ackson Mwansasu alipomtembelea leo ofisini kwake.
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt Tulia Ackson Mwansasu akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini
Bi.Yasemin Eralp alipotembelea ofisi za Bunge Jijini Dar es salaam leo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu(kulia) akimuelezea jambo
Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin Eralp (katikati) na kushoto ni
Katibu wa Balozi huyo Bw.Berat Colak
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt Tulia Ackson Mwansasu (Kulia) pamoja na maofisa wa Bunge waliokaa
kushoto wakizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin Eralp (wa
pili kulia) na kushoto wa Balozi ni Katibu wa Balozi huyo Bw.Berat Colak
(Picha zote na Raymond Mushumbusi Maelezo)
……………………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi- Maelezo
Serikali ya Uturuki imeahidi kuisaidia
Serikali ya Tanzania kufanikisha mpango wa utoaji wa elimu bure kwa
wanafunzi utakaoanza January mwakani.
Hayo yamezungumzwa leo na Balozi wa Uturuki
nchini Bi Yasemin Eralp alipokuwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu
alipomtembelea ofisini kwake.
Balozi yasemin Eralp ameainisha Serikali ya
Uturuki imekuwa ikisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali nakuwa na
ushirikiano wa Mabunge ya nchi hizo mbili ambao umeongeza mahusianio
mazuri ya nchi hizo, mbali na ushirikiano wa Bunge ameweka wazi kuwa
serikali yake ya Uturuki inaweza kushirikiana na Serikali ya Tanzania
kuwezesha miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, ujenzi wa
maktaba za shule,ujenzi wa viwanda na ujenzi wa vituo vya Afya na
Hospitali nchini.
“ Katika kuunga mkono mpango wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa elimu bure kwa watanzania
kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari tuko tayari kushirikiana na
serikali kwa kutoa msaada wa vifaa kwa wanafunzi kama vile vitabu,
kompyuta na kujenga maktaba katika shule mbalimbali”alisema Balozi
Eralp.
Naye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu ameishukuru Serikali ya
Uturuki kwa kusaidia Tanzania katika miradi ya kimaendeleo na kuzidi
kuomba ushirikiano zaidi toka kwao hasa katika maswala ya Bunge katika
nchi hizo.
“ Tunaishukuru Serikali ya Uturuki kwa
ushirikiano wao katika maswala ya Bunge na kujenga mahusiano mazuri na
Tanzania na hata katika miradi ya maendeleo ya jamii inayofadhiliwa na
serikali ya Uturuki na tunaomba tuendeleza mahusiano zaidi katika
mahusiano ya mabunge ya nchi hizi mbili ” alisema Dkt Tulia.
Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na
Uturuki katika maswala ya Bunge na mwaka 2010 wawakilishi toka Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia chini ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo
Mhe. Samwel Sitta walitembelea Bunge la Uturuki kwa mwaliko wa
aliyekuwa Spika wa Bunge la Uturuki wakati huo Mhe. Mehmet Ali Sahim.


0 comments :
Post a Comment