Mkurugenzi
wa Mipango, Sera na Utafiti Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB),
Francis Assenga (Kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kuwekeana saini
makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB. Kulia ni
viongozi waandamizi wa TADB na PASS.
Mkurugenzi
wa Biashara na Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Robert Pascal (Katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kuwekeana
saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB. Kulia ni
viongozi waandamizi wa TADB na PASS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango,
Sera na Utafiti wa TADB, Bw. Francis Assenga (Kushoto) na Mkuu wa Sheria
na Huduma wa Benki hiyo, Bibi Neema Christina John (Kulia).
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas
Samkyi (Kushoto) akizungumza kabla ya kutiliana saini makubaliano
yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS.
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay.
Mkurugenzi
Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Katikati) akizungumza kabla ya
kutiliana saini makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB
kupata dhamana kutoka PASS. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi na Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Biashara wa PASS, Bw. Killo Lussewa (Kulia).
Wanahabari wakiwajibika wakati wa hafla ya kuwekeana saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas
Samkyi (Kushoto) akitia saini makubaliano yatakayowezesha wakulima
wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Katkati ni Mkurugenzi Mkuu wa
PASS, Bw. Nicomed Bohay na na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa
PASS, Bw. Killo Lussewa (Kulia).
Mkuu
wa Sheria na Huduma wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),,
Bibi Neema Christina John (Kushoto) akigonga muhuri makubaliano
yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS.
Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa
PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia).
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas
Samkyi (Kushoto) akibadilishana hati za makubaliano yatakayowezesha
wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS na Mkurugenzi Mkuu wa
PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia).
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas
Samkyi (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia)
wakionesha hati za makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB
kupata dhamana kutoka PASS katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya
TADB.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
BANKI
ya Maendeleo Kilimo nchini (TADB) imesema kuwa wakulima imewataka
wakulima wadogo wajiunge katika vikundi ili waweze kupata mikopo yenye
masharti nafuu ya kuendeleza kilimo ambacho kitawabadilisha kiuchumi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati makubaliano ya
kati ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Taasisi ya Sekta Binafsi
ya Kusaidia Wakulima (PASS), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Thomas
Samkyi amesema kuwa wakulima wakitumia benki hiyo watakwamka na
umasikini kutokana na kulima kilimo chenye tija.
Amesema
kuwa kwa wakulima wakiwa na vigezo watapata mkopo kutokana na benki
hiyo iko kwa ajili yao katika kuendesha kilimo chenye tija katika
kuondokana na kilimo cha kujikimu.
Samkyi amesema kuwa PASS kutoa udhamini kwa wakulima watasidia benki kutoa mikopo kwa kutokana dhamana hiyo.
Mazao
ambayo yanapata mkopo katika benki hiyo ni Mpunga,Mahindi,Mazo ya
Misitu, Ufugaji, Usindikaji Alizeti,Uwere isipo kuwa tumbaku.
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa PASS, Nicomed Bohay amesema kuwa kuanza na
udhamini kwa wakulima wametenga bilioni tatu kadri wanavyokwenda na
benki hiyo wataongeza udhamini huo.
Amesema
kuwa udhamini waliofanya katika kipindi kilichopita wakulima wameweza
kukua kiuchumi kwa kubadilisha maisha kutokana na kilimo.
Aidha
amesema kuwa katika makubaliano hayo ni kwa miaka mitano na baada ya
kuisha wanaweza kuendelea ikiwa ni lengo la kusaidia wakulima kukua
kiuchumi.
0 comments :
Post a Comment