Halmashauri
ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani imeahidi kuwalipa wananchi wanaostahili
kulipwa fidia ya ardhi ambayo ilichukuliwa na Serikali kwa lengo la
kutekeleza mradi wa kitovu cha Mji wa Kibaha (CBG) unaotegemewa kujengwa
katika eneo la Machinjioni.
Akizungumza
kuhusiana na madai ya wananchi wa eneo la Machinjioni Mjini Kibaha,
Afisa Habari wa Halmashauri ya Mji huo Innocent Byarugaba amesema
Halmashauri hiyo ipo katika maandalizi ya kuitisha kikao na wananchi wa
eneo la Machinjioni ili kufanya tathmini ya wanaostahili kulipwa na
kuanza utaratibu wa kuwalipa.
Amefafanua
kuwa zoezi la kufanya tathmini katika eneo hilo lilishindikana kutokana
na wafanya tathmini kufanyiwa fujo hivyo kukwamisha utekelezaji wa
zoezi hilo kwa wakati.
“
Kabla eneo hili la Machinjioni halijabadilishwa matumizi kutoka kuwa
eneo la viwanda na kubadilisha kuwa eneo la mradi wa kitovu cha Mji wa
Kibaha (CBG), Halmashauri haikuwahi kutoa kibali kwa mwananchi yoyote
kuendeleza eneo hilo na wale wanaodai kuwa eneo hilo ni lao ni wavamizi
na Halmashauri inafanya ustarabu tu kuwalipa wale walioendeleza ili
kuondoa malumbano yaliyopo,” alisema Byarugaba.
Aidha
Halmashauri ya inaendelea kupima eneo la Machinjioni kwa hilo kwa ajili
ya kuwalipa fidia wananchi ili kupisha utekelezaji wa mradi huo.
Innocent
Byarugabana amewaasa wakazi wa Mji wa Kibaha kutovamia maeneo na
kuyaendeleza bila kuwa na hati ya umiliki wa eneo husika.
Halmashauri
ya Mji wa Kibaha ipo katika mikakati ya kuendeleza maeneo ambayo yapo
katika mikakati ya kufanyiwa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na
kuhakikisha Sheria ya 2007 ya uendelezaji wa Miji ya mwaka 2008
inatekelezwa.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO


0 comments :
Post a Comment